Friday, 7 February 2014

Uchaguzi kata ya nyasura wilaya ya bunda hatarini kutokufanyika?

UCHAGUZI KATA YA NYASURA WILAYA YA BUNDA HATARINI KUTOKUFANYIKA.


Uchaguzi wa kata ya Nyasura wilaya ya Bunda hatarini kutokufanyika.

Kwa nini?!

1. Nia ni kutaka kumuokoa Mh Wassira na ccm kwa aibu watakayovuna. Kumbukeni wassira alisema chadema inakufa kabla ya 2013, hivyo kushinda kwa chadema kwenye kata hiyo ni sawa na kudhihirisha kuwa Wassira alitumika/anatumika kama tarumbeta la Propaganda.

CCM washambulia mwandishi wa habari vibaya, amri ya Nape? IGP Mangu here is the test

Nimelazimika kukatisha safari baada ya kusikia taarifa za CCM kuanza kutekeleza agizo alilolitoa Nape Nnauye leo mjini Mwanza kwamba Green Guard waanze kufanya kazi yao. Kweli wameanza. Muda mfupi uliopita, Mwandishi wa Habari Christopher Maregesi amepewa kipigo kikali na CCM, huko Bunda. Ilikuwa ni baada ya kitu kinachodaiwa au kuonekana kuwa nimtego kumnasa, kisha watu wa Green Guard, wanaopewa mafunzo kwenye makambi ya CCM yanayoanzishwa kila wakati wa uchaguzi, wakafanya kazi yao.

Baregu aonya kuhusu Bunge Maalumu

8E9U6011
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu amesema, Bunge maalumu lijao la Katiba linaweza kugeuka kituko iwapo wajumbe wake wataweka mbele masilahi ya vyama vya kisiasa na kuacha misingi ya kujenga taifa moja na lenye mshikamano. Pia amesema, pamoja na Tume hiyo ya Mabadiliko ya Katiba kukamilisha kazi yake lakini kwa upande mwingine hatakubali kukaa kimya pindi atakapoona kazi nzuri iliyofanywa ya ukusanyaji maoni ya wananchi ikidhihakiwa.

Mbowe hana shahada ya Chuo Kikuu?

Katika mkutano wa chadema wa M4C pamoja daima uliofanyika tarehe 27 january 2014 ktk viwanja vya barafu jamhuri Dodoma mjini, Tundu Lissu alisema Yafuatayo ..."Ni kweli kuwa mwenyekiti wetu Mbowe hana shahada ya chuo kikuu lakini hiyo sio sababu ya kumnyima uongoz". alisema Lissu juu ya elimu ya Mbowe.

Mbunge Msigwa afikishwa kortini akidaiwa kujeruhi

MBUNGE wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumjeruhi kada wa Chama Cha Mapunduzi (CCM) kwa kitu kitu kizito. Mchungaji Msigwa  alifikishwa  katika mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa, Godfrey Isaya jana na kusomewa shitaka moja la kujeruhi. Akisoma shitaka hilo Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Elizabeth Swai alidai Mchungaji Msigwa alitenda kosa hilo Febrauri 5, 2014 katika kijiji cha Nduli  mjini Iringa. 

Kikwete awaonya wanasiasa

Rais Jakaya Kikwete ametangaza kuwa Bunge Maalumu la Katiba litaanza Februari 18 mwaka huu huku akiwataka viongozi wa vyama vya siasa nchini kuweka mbele masilahi ya Taifa na siyo ya vyama vyao. Rais Kikwete alisema wajumbe 640 wa Bunge hilo wengi ni wafuasi wa vyama vya siasa, hivyo wanatakiwa kukubaliana kwa hoja badala ya kila upande kuvutia kwake.Aliwaonya pia wanasiasa kutokazania suala la muundo wa Muungano peke yake, bali waangalie na masuala mengine yaliyomo kwenye rasimu hiyo ambayo ni muhimu kwa Taifa.

Lema ajisalimisha polisi


MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) amejisalimisha mikononi mwa  polisi mkoani hapa baada ya kutakiwa kwenda kuandika maelezo ya uharibifu wa mali. Lema aliwasili kituoni hapo jana mchana akiongozana na Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Arusha Efatha Nanyaro na viongozi wengine na kuelekea kwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha, OCD Gileas Mroto.

Wednesday, 5 February 2014

Urais CCM kama vita

“Mungu amempa uwezo akisimama watu humfuata nyuma katika kusaidia wanyonge, yeye ana nguvu za Mungu, nadhani hiyo ndiyo inamletea taabu. Sasa mimi niulize kuna kamati za maadili sawa, tangu mwaka 1993 ameanza harambee leo wanasema ameanza kampeni?” alihoji Nangole. Alisema Lowassa amekuwa akisaidia kila pembe ya nchi katika nyumba za ibada na hafanyi kampeni, kwani hao wanaosaidiwa siyo wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM.

Lema Vs Polisi tena Arusha

Polisi mkoani hapa, imetoa notisi ya kukamatwa kwa Mbunge wa Arusha, Godbless Lema (pichani) na wenzake watatu ili kuhojiwa kuhusu malalamiko ya vurugu zilizotokea kwenye mikutano ya kampeni za uchaguzi wa kiti cha udiwani Kata ya Sombetini, wiki iliyopita na kusababisha watu kadhaa walijeruhiwa. Hata hivyo, Mbunge Lema alisema jana kuwa hana taarifa ya kutafutwa polisi kwa ajili ya mahojiano. Alisema kama ni kweli anatafutwa basi taratibu zifuatwe ili aweze kwenda kuripoti polisi.

Tuesday, 4 February 2014

KUMBE LOWASSA NI TISHIO CCM

PATASHIKA nguo kuchanika ni kauli ya kibabe inayoweza kutumika kuelezea sakata la siasa za makundi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM)  linaloshika kasi huku baadhi ya wanachama wakitupiana lawama kwa kuunga mkono upande fulani kuelekea mbio za urais hapo mwakani. Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Ngoyai Lowassa hajawahi kutoa tamko lolote juu ya kugombea urais mwakani lakini shutuma kwamba anautaka zimekuwa zikiibuka kila kukicha.

Njombe: Kada wa CHADEMA avunjwa taya, watatu wawekwa ndani

INASIKITISHA LAKINI IMETOKEA

Katika hali isiyotarajiwa kamanda mmoja wa chadema mkoani njombe amevunjwa taya leo hii katika eneo la matalawe kwenye jimbo la Mama ANNA MAKINDA.

Haya yametokea baada ya kamanda huyo ambaye ni kiongozi wa ulinzi kanda ya nyanda za juu kusini bwana KALONGA kuwafumania viongozi wa chama cha MAPINDUZI wakigawa fedha kwa wananchi ili wawapatie vitambulisho vyao vya kupigia kura.

Kalonga na viongozi wengine walizingirwa na viongozi wa chama mapinduzi na kuanza kupokea kipigo kitakatifu ambacho kilipelekea taya zake kuvunjika vibaya.

polisi walipofika waliwakamata na kuwapeleka kituoni ambapo viongozi watatu wamewekwa ndani huku aliyeumizwa akakicheleweshwa kwa makusudi kupelekwa hospitali huku wakitoa kauli zilizokosa ubinadamu.

Anayeratibu zoezi hili kwa karibu kabisa ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa na mbunge wa jimbo la njombe kaskazini bwana ja people ambaye mudda wote yupo karibu a polisi ili kuhakikisha wanaihujumu chadema

Nitaendelea kuwapa taarifa kwa kadiri ninavyoweza ila kwa sasa narudi polisi kupigania kamanda wetu atoke ili akatibiwe

MUNGU ISIMAMIE CHADEMA

MUNGU ITAZAME TENA TANZANIA


Mpinzani Mpya wa Mwigulu apatikana

Ni Mwanasheria machachari George Kidindima ametangaza nia ya kugombea Ubunge ktk Jimbo la iramba magharibi 2015 kupitia CHADEMA -Kidindima amepata kuwa Mhadhiri msaidizi ktk Chuo ya uhasibu Singida campus pia ni mwandishi wa vitabu kadhaa vya business law.

Stay tune...............

Msekwa: Wapinzani wakiungana wanaweza kuing’oa CCM

Kiongozi Mstaafu wa CCM, Pius Msekwa amesema endapo vyama vya upinzani vikiungana na kuweka mikakati makini ya muda mrefu, vinaweza kuking’oa CCM madarakani. Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na mwandishi wetu jana, Msekwa alisema kwa mtindo wa sasa wa vyama vya upinzani kila kimoja kusimama peke itakuwa ndoto kukishinda CCM. “Kama vyama vya upinzani vinataka kuwe na upinzani wenye nguvu dhidi ya CCM ni lazima viungane vyote. Tena viweke mikakakati ya muda mrefu ya kujiimarisha,” alisema Msekwa kwenye mahojiano hayo. 

CHADEMA wataendelea kutugawa na kutubagua hadi lini?

CHADEMA na ubaguzi ulipitiliza kikomo,walianza na ubaguzi wa ukabila na ukanda ambao kilasiku wanasema ni propaganda za ccm,wakatufundisha watanzania tuvibague vyombo vya habari TBC,UHURU,RAIA MWEMA,MWANANCHI,MTANZANIA,JAMBO LEO NA STARTV.

Wakaendelea tena tumbague ZITTO KABWE tusishiriki na Zitto wala mikutano yake,huko nyuma walitufundisha tuibague nchi yetu na Rais wetu wakati tunaishi Tanzania sijui walitaka tuhamie Rwanda sijui? walitufundisha tuwabague wapinzan bungeni CUF,TLP,UDP NA NCCR.

Leo hii wanatuhamasisha tuwabague wasanii waliojiunga CCM Kweli ni sawa?kesho mtatuambia tusiende Zanzibar sababu kiembesamaki mmepata kura 34,je hamuoni Sudan kusini leo wanabaguana wao kwa wao tena? Acheni dhambi ya ubaguzi sisi ni watanzania tushindane kwa hoja,

Uhamiaji watuhumiwa kuhujumu mgombea Chadema

Mgombea udiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika uchaguzi mdogo kata yaKiboriloni, Manispaa ya Moshi, Frank Kagoma, ameitwa na Idara ya Uhamiaji mjini hapa kwenda kuthibitisha uhalali wa uraia wake ambao unatiliwa shaka. Hata hivyo, Kagoma ambaye anawania kiti hicho akichuana vikali na mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Willy Tulli na mgombea wa UDP, Adon Mzava, amesema hayuko tayari kuitikia wito huo kutokana na kushauriwa na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, kutokwenda hadi hapo chama kitakapotoa maelekezo.

Mbowe amjibu Kikwete

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), FreemanMbowe amemjibu Rais Jakaya Kikwete kwamba asiingize utani katika masuala mazito ya taifa. Mbowe alisema Katiba ya Tanzania, itaamuriwa na wananchi wenyewe na si Chama Cha Mapinduzi (CM) ambacho kimekuwa na mkakati mkali wa kutaka kuua maoni ya wananchi. Mbowe ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja tu baada ya Rais Kikwete kudai amesikia kiongozi huyo wa upinzani akitangaza kutumia nguvu kupata Katiba mpya.

Rais Kikwete: Wanasiasa acheni kuingilia masuala ya kitaalam

Rais Jakaya Kikwete amewataka wanasiasa kuacha kutoa majibu ya kisiasa katika masuala na changamoto za kitaalam na kiufundi. Amesema matatizo na changamoto za kitaalam na kiufundi ziachiwe kutafutiwa majawabu ya kiufundi badala ya kupatiwa majawabu ya kisiasa. Rais Kikwete alitoa rai hiyo mwishoni mwa wiki, wakati akizungumza na wajumbe wa Halmashauri ya CCM ya Mkoa wa Mbeya. 

Friday, 31 January 2014

Kuna ukweli wowote hapa?

Malecela amvaa Edward Lowassa

  • Ni mbio za urais 2015
  • Amtuhumu kumwaga fedha
Makamu Mwenyekiti mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samuel Malecela, akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) moja ya fulana iliyoandikwa Friends of Edward Lowassa (Marafiki wa  Lowassa)

Tuesday, 28 January 2014

Hivi kwa nini wabunge wa CHADEMA wanakuwa waongo waongo?

Wakuu,mimi huwa nakereka sana ninapohudhuria mikutano ya baadhi ya wabunge wa CHADEMA.

Nianze hivi,
Ukienda jijini mbeya karibu eneo kubwa la barabara za mitaa zimepigwa lami,sasa BWANA JOSEPH MBILINYI anajitapa kuwa yeye ndo aliyeleta hiyo lami kana kwamba alitoa pesa yake mfukoni. Jamani,hizi barabara ni mpango wa uboreshaji wa majiji na bado ilikuwa ni utekelezaji wa ilani ya chama kilichopo madarakani.

Hatimaye Mh, January Makamba atimiza umri wa kugombea Urais

Leo 28/January 2014, kijana na mwanasiasa machachari na mwenye maono makubwa ya kiongozi ndugu January Makamba ametimiza miaka 40 ambao ni umri unaotakiwa kikatiba kugombea urais

Mbowe apaisha homa serikali 3

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema iwapo kutakuwa na uchakachuaji wa rasimu ya Katiba mpya na kuondoa mapendekezo ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya mfumo wa serikali tatu, chama hicho hakitakubali na hatua madhubuti zitachukuliwa. Mbowe aliyasema hayo jana kwenye mkutano wa hadhara wakati akihutubia maelfu ya wakazi wa Biharamulo mkoani Kagera na Chato, mkoani Geita. 
  • Sugu atamba maofisa wake hutoa siri kwao
  • Asema ni kutokana na Serikali kutokuwa makini
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema mafanikio kinayopata yanatokana na maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa kutoa siri kwao. Kauli hiyo imetolewa juzi mjini hapa na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu), wakati akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Viwanja vya Ruanda, Nzovwe.Alisema hatua ya nchi kuyumba, inatokana na Serikali kutowajali maofisa wa Idara hiyo, hali inayowalazimu kuvujisha siri kwao.

Mbunge awezesha vikundi vya wanawake

Mbunge wa viti Maalum (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, Betty Machangu, amewashauri wananchi na vikundi vya ujasiria mali vya kinamama na vijana mkoani humo kuhakikisha wanajiunga katika vikundi ili iwe rahisi kupata misaada ya kuinua vipato vyao kutoka serikalini na baadhi ya taasisi mbalimbali nchini.  Machangu aliyasema hayo juzi mkoani Kilimanjaro katika ziara yake ya kuhamasisha vikundi vya wajasiriamali na kutembelea vikundi vyote vilivyopo katika Wilaya ya Moshi Vijijini na kuvipatia fedha baadhi ya vikundi.

Monday, 27 January 2014

Vicent Nyerere:Ukimtumia polisi sms ya tafadhali nipigie,atakujibu kwa sms ya niongezee salio!

Akiongea muda huu katika kipindi cha ITV cha "dakika 45" waziri kivuli wa mambo ya ndani,mh.Vicent Nyerere (pichani) ametoa kali kwa kusema kutokana na ugumu wa maisha unaowakabili polisi wetu leo hii ukamtumia polisi ujumbe wa "tafadhali nipigie",yeye atakujibu kwa ujumbe wa "tafadhali niongezee salio"!

Tuhuma Baraza la Mawaziri

  • Lipumba atilia shaka elimu ya waziri wa fedha
  • Yeye amjibu kwa kutoa vielelezo lukuki 
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amelishushia tuhuma nzito Baraza la Mawaziri, baada ya kudai baadhi ya mawaziri walioteuliwa hawana elimu ya kutosha.  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema mmoja wa mawaziri hao ni Waziri wa Fedha, Saada Mkuya.Alisema chama chake, kina wasiwasi na elimu ya Waziri Mkuya, kutokana na wasifu wake kutoonyesha vyuo alivyosoma wakati wa kupata shahada ya kwanza na ya pili katika masuala ya biashara.

CHADEMA hamuwezi kutwaa dola kwa Chopa na Maandamano, waelezeni wananchi mtawafanyia nini

Wanaukumbi.

Chama chochote makini lengo lake ni kutwaa dola, kutwaa dola kuna kuja baada kuwaeleza wananchi nini dhumuni lenu kama chama cha siasa, wananchi wanataka kufahamu mtawafanyia nini kama wakiwachagua kuingia Ikulu, kwenye masuala muhimu Afya, Elimu, Kilimo, Uchumi wa Nchi, Mahusiano ya Kimataifa, Ajira kwa Vijana, tatizo la watanzania siyo Chopa wala maandamano.

VYAMA VYA SIASA VINAPIGA TEKE MASLAHI YA UMMA!

Hakika kujikwaa ni jambo la bahati mbaya kwa mtembezi aliye makini na ni jambo la kawaida kwa mtembezi asiye makini! Na ni mtembezi makini pekee ambaye atathubutu kujiuliza pale atakakapokuwa amejikwaa, yule asiyekuwa makini hatojiuliza kamwe.Tangu kuingia kwa muhula wa pili wa Serikali ya awamu ya nne, Watanzania wameshuhudia matukio ya kushtusha mno ndani ya vyama vya siasa.Vyama vya siasa vimekuwa vikitoa maamuzi ambayo yamekuwa yakivuruga maslahi ya wananchi wapiga na kuacha sononeko kwa umma.

Umejifunza nini kupitia picha hizi?

Mbowe: Niko tayari kwenda jela kwa kudai katiba mpya

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeendelea na ziara zake za Operesheni Movement For Change (M4C) na ‘Pamoja Daima katika maeneo kadhaa nchini huku viongozi wake wakuu wakizungumzia mambo makuu yanayoikabili nchi. Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, akiwa mkoani Kagera, alisema yuko tayari kuwa wa kwanza kufungwa kwa kosa la kudai katiba mpya itumike ikiwa serikali italazimisha kuendelea kutumia katiba ya zamani.

Friday, 24 January 2014

CCM yamgeukia Balozi Sefue

  • Yadai kauli yake kwa mawaziri mizigo ina ukakasi

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimempinga Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, kutokana na hatua ya kuwatetea baadhi ya mawaziri mizigo waliorudishwa tena kwenye Baraza la Mawaziri, huku kikisema kauli yake ina ukakasi. Msimamo wa CCM umekuja siku chache, baada ya Balozi Sefue kutangaza mabadiliko ya Baraza la Mawaziri na kuwatetea mawaziri mizigo kwa kile alichosema hawapaswi kulaumiwa kutokana na wakati mwingine kucheleweshewa fedha kwenye wizara zao.

CHADEMA,Zitto ,Mbowe na 48 LAWS OF POWER

Hapa JF tuliwahi kumjadili Kikwete zamani kwa kutumia kitabu hiki maarufu '48 laws of power'
http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la...r-2-print.htmlleo ningependa tukitumie kitabu hiki kujadili yaliyotokeaCHADEMA hasa kwa Zitto na Mbowe na viongozi wote kwa kutumia kitabu hiki.....
  • Je ni sheria zipi Zitto alizitumia vizuri au alishindwa kuzitumia?
  • Mbowe aliweza zipi? zipi alishindwa na wengineo mfano kina Lissu na Mnyika na Lema wana tumia zipi na zipi wanashindwa...
................naamini itakuwa kitu cha kujifunza kwa kila mtu................

Mikutano ya M4C - Operesheni Pamoja Daima, Kigoma, Mbeya, Rukwa, Manyara na Arusha

Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe akiongoza maaandamano Kuelekea Himo kwenye Uzinduzi wa Operesheni Pamoja Daima 

CHADEMA Arumeru mashariki jana : Lissu, Nassari na Heche watisha.

Mamilioni ya Lowassa yaingia CHADEMA?

Katika kile kinachoonekana kujihakikishia Urais 2015 aliyewahi kuwa waziri mkuu (sio waziri mkuu mstaafu kwani uwaziri sio nafasi ya kuajiriwa na kisha kustaafu) ndugu Lowasa ameanza ama anaendeleza kazi ya kuwamgia mamilioni viongoz wakuu wa chadema katika kumsafishia njia. Najua suala hili litashtusha wengi lakini ndio uhalisia kwani tangia mwaka 2010 viongozi wa kitaifa wa CHADEMA wamebakia kuwaandama viongozi wengine wa CCM huku wakifumbia madudu na uchafu anaoendelea kuufanya Lowasa kama kwamba hawaoni hadi hatua ya wanachama na wapenzi kuanza kuhoji kwa nn Lowasa hazungumziwi? ambapo majibu rahisi na yasiyo na mshiko kutoka kwa viongozi wa chama ni kwamba Lowasa kwa kuwa atapishwa na CCM mwaka 2015 kugombea urais sio sawa kumzungumzia kwa sasa kwani kutampa mwanya wa kujisafisha katika kashfa zake na hivo kukosa hoja za kumchafua kwa wananchi kama ilivyo kawaida ya siasa za Tanzania ili upendwe unatengeza fitina mwenzio achukiwe.  ukweli ni kwamba Lowasa amekuwa akiwapa mamilioni viongozi hao ili kuwadhoofisha wapinzani wake na hatimaye kujihakikishia kupitishwa na chama chake kugombea uraisi.

Zitto ruksa kukata rufaa Chadema

Uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) umempelekea Zitto Kabwe taarifa ya kikao cha Kamati Kuu kilichomvua madaraka yake ndani ya chama hicho ili aweze kukata rufaa. Habari za kutoka ndani ya Chadema zinaeleza kuwa Kamati Kuu ya chama hicho ilifikia uamuzi huo wakati wa vikao vyake vilivyofanyika kati ya Januari 3 na 4, mwaka huu. Kutokana na uamuzi huo, Zitto sasa ataweza kukata rufaa ya kupinga kuvuliwa madaraka kwenye Baraza Kuu la chama hicho.

Uteuzi wa Kikwete waikoroga CCM

Uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete kuwaacha katika Baraza la Mawaziri, mawaziri wote waliotajwa na CCM kuwa wameshindwa kutekeleza majukumu yao umekichanganya chama hicho, baada ya jana kusema kuwa hakitasita kuchukua hatua kali dhidi ya mawaziri hao na wengine, iwapo watashindwa kurekebisha upungufu wa kiutendaji unaozikabili wizara zao.

Balozi Ali Abeid Karume: “Tunataka Serikali mbili, kuujenga Muungano wetu”.

ali karume
BALOZI Ali Abeid Aman Karume (pichani) ambaye pia ni MNEC wa Chama cha Mapinduzi CCM, Amesema Taifa linaitaji muundo wa Serikali mbili ilikuujenga Muungano thabitio uliasisiwa na viongozi wakuu ambao wameufikisha hapa ilipo sasa. Balozi Ali Karume alisema hayo jioni ya leo (Januarin23) kwenye mkutano wa hadhara wa kumnadi Mgombea wa nafasi ya Uwakilishi kwa chama hicho kupitia jimbo la Kiembesamaki, Mahmoud Thabit Kombo, ambapo aliwataka wanakiembe samaki kumchagua mgombea huyo ilikwenda kuwatetea na kuwatumikia katika kuunda mambo mbalimbali ikiwemo suala hilo la Muungano na Serikali mbili.

Chadema yawasilisha pingamizi dhidi ya Zitto

Mawakili wa chama CHADEMA, Tundu Lissu (kushoto) na Peter Kibatala

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimewasilisha majibu na pingamizi la awali dhidi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kuhusu Kamati Kuu ya Chama hicho akiitaka mahakama kuzuia uanachama wake usijadiliwe hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa. Kadhalika, chama hicho kimejibu barua ya Zitto pamoja na kuwasilisha mwenendo wa shauri lililopelekea kuvuliwa nyadhifa za uongozi katika chama hicho kama mlalamikaji alivyoomba.

Thursday, 23 January 2014

Chadema yawaonya wabunge CCM

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amesema kuwa chama hicho kitachukua uamuzi mgumu ikiwa wabunge wa CCM watajikita katika kulinda masilahi yao kwenye Bunge Maalumu la Katiba kinyume na maoni ya wananchi. Alisema hayo jana katika Wilaya ya Nyasa na Mbinga kwenye siku ya kwanza ya Operesheni Pamoja Daima. Katika operesheni hiyo, ambapo aliruka kwa helikopta katika sehemu mbalimbali, alihutubia mikutano katika maeneo ya Mbamba Bay, Mbinga, Peramiho, Namtumbo na Songea Mjini.

JK kufyeka 2,500 Bunge la Katiba

  • Ni asilimia 7.4 tu watakaopenya
  • Majina hadharani mapema wiki ijayo
Majina ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete sasa yatawekwa hadharani wiki ijayo. Hata hivyo, Rais Jakaya Kikwete atakuwa na mtihani mgumu wa kuteua majina ya wajumbe hao kutoka asasi mbalimbali kutokana na idadi kubwa ya majina yaliyowasilishwa Ikulu na asasi hizo kulingana na nafasi ndogo za kuteua. Jumapili iliyopita, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema kuwa majina ya watu 2,722 yaliyowasilishwa kwa Rais kutoka makundi hayo yalikuwa yanaendelea kuchambuliwa.

Ufafanuzi wa CCM kwa umma kuhusu “Mawaziri mizigo”

Mara baada ya kuundwa kwa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa inayoongozwa na Katibu Mkuu Ndg. Abdulrahman Kinana mwanzoni mwaka mwaka jana, Sekretarieti hiyo imejiwekea utaratibu wa kufanya ziara mikoani kukutana na wananchi kusikiliza kero zao,kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuimarisha Chama mikoani. Utaratibu huu ni agizo la mkutano mkuu wa Taifa wa nane wa CCM uliofanyika Novemba 2012 mjini Dodoma. Nanukuu azimio hilo;

Wednesday, 22 January 2014

Ratiba ya M4C- Operesheni Pamoja Daima, Ruvuma, Tabora na Tanga

Kama ambavyo jana umma wa Watanzania ulitaarifiwa kupitia kwenye mkutano wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe na wanahabari, Chama leo kinaanza operesheni ya takriban wiki mbili kwa nchi nzima (mijini na vijijini). Kuna jumla ya timu 6 zilizoko uwanja wa mapambano kuendesha M4C- Operesheni Pamoja Daima, ambazo zote zinaanza kazi leo katika maeneo zilizopangiwa. Timu tatu zitakuwa zikishambulia kutokea angani na timu tatu zitakuwa zikisonga mbele nchi kavu.

Prf,Lipumba:Kiembe samaki mchagueni mgombea wa CUF ayaendeleze aliyoyaacha Mansour

Mgombea wa nafasi ya uwakilishi jimbo la kiembe samaki Bwana Abdull Malik Haji akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Chama Taif Prf.Lipumba baada ya kukabidhiwa manufesto ya chama.
Mgombea wa nafasi ya uwakilishi jimbo la kiembe samaki Bwana Abdull Malik Haji akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Chama Taif Prf.Lipumba baada ya kukabidhiwa manufesto ya chama.[/captio0n]Chama cha Wananchi CUF kimesema hakiutokuwa tayari kudhulumiwa na kufanyiwa hujuma kama zilizofanywa katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Bububu.

Raza awang’akia wanaotaka atimuliwe uanachama CCM

Zanzibar. Mwakilishi wa Jimbo la Uzini (CCM), Mohamed Raza Dharamsi amesema hakuna kifungu wala mwongozo wowote wa CCM unaomzuia mwanachama kutotumia demokrasia ya kukosoa ikiwemo muundo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Raza alitoa msimamo katika majibu yake ya maandishi alipotakiwa kujieleza mbele ya kamati ya siasa ya jimbo na wilaya huko Uzini Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja hivi karibuni.

Mbunge wa Chalinze , Said Bwanamdogo , CCM , afariki dunia

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne S. Makinda (Mb), anasikitika kutoa taarifa ya kifo cha Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Saidi Ramadhani Bwanamdogo Kilichotokea leo (Jumatano) asubuhi tarehe 22.1.2014 Katika hospitali ya Muhimbili/MOI alikokuwa amelazwa kwa Matibabu. 

Mipango ya Mazishi zinaendela kufanywa na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya Marehemu, ambapo mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho siku ya Alhamisi tarehe 23 Januari, 2014 kijijini kwake MIONO, Wilaya ya BAGAMOYO, Mkoa wa PWANI. Taarifa zaidi juu ya msiba huu zitaendelea kutolewa na Ofisis ya Bunge kadrizitakapopatikana.

Inna llilah Waina Illaih Rajiun!”

Imetolewa na
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusianao wa Kimataifa,
Ofisi ya Bunge,
DAR ES SALAAM

22.01.2014.

RASIMU YA KATIBA KUCHAPWA GAZETI LA SERIKALI IJUMAA HII

Kifungu 20 (2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura 83, Toleo la 2013 inamtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuchapisha kwenye Gazeti la Serikali Rasimu ya Katiba ndani ya siku thelathini (30) baada ya kukabidhiwa rasimu hiyo na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue inaeleza kwamba, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, alikabidhiwa Rasimu ya Katiba tarehe 30 Desemba, 2013, na ataichapisha kwenye Gazeti la Serikali litakalotolewa Ijumaa, tarehe 24 Januari 2014.

Mnyika amvaa Magufuli

Mbunge wa Jimbo la Ubungo (Chadema), John Mnyika amemtaka Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli na Wakala wa Barabara (Tanroads) waelekeze nguvu katika kusimamia ujenzi wa mradi wa mabasi yaendayo kwa haraka (BRT) kutoka Ubungo hadi Chalinze. Amemtaka Waziri Magufuli pia kuipitia, kuiheshimu na kuwezesha utekelezaji wa maamuzi ya mahakama juu ya hukumu ya kesi ya wananchi wa maeneo hayo ambao wanapinga kuondolewa kupisha ujenzi wa barabara hiyo.

Chadema kutikisa nchi; Helikopta tatu kurushwa nchi nzima

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuanzia leo, kinarusha helkopta tatu kwa siku 14 mfululizo, katika  kutekeleza kampeni iliyopewa jina la Operesheni Pamoja Daima (ODB) itakayoendeshwa katika mikoa yote nchini. Ziara hiyo inaanzia katika mikoa ya Tanga, Mwanza na Ruvuma, huku viongozi wa chama hicho wakijigawa katika makundi sita; matatu yakitumia helkopta na matatu yatawafikia wananchi kwa kutumia usafiri wa magari. 

Monday, 20 January 2014

Umejifunza nini kupitia hizi picha?

Sikurudisha fomu kwa kuwa CHADEMA imepoteza mwelekeo

Aliyetarajiwa kuwa mgombea wa udiwani wa Kata ya Mtae wilayani Lushoto kupitia CHADEMA na kutojitokeza kurejesha fomu hatimaye amejisalimisha polisi. Mgombea huyo, Ali Said Jaha alijisalimisha juzi Jumamosi asubuhi katika Kituo cha Polisi cha Lushoto na kutoa maelezo kwamba hakuwa amepotea kama ilivyokuwa imeenezwa kwenye mitandao ya kijamii.Alisema wakati wa kurejesha fomu siku ya Alhamisi Januari 16 mwaka huu kulikuwa na matatizo ya kifamilia nyumbani kwake hivyo ikamlazimu kuyapa kipaumbele hatimaye akajikuta akiwa amechelewa kuwasili ofisi za Kata ya Mtae.

Hali bado tete CHADEMA


  • CHADEMA HALI BADO TETE.
  • SASA NI MBOWE vs SLAA.


Baada ya kutokufanikiwa kumvua uanachama wake na kufanikiwa kumvua nyadhifa zake zote ndani ya chama na ndani ya bunge sasa hali sio nzuri ndani ya chama na hasa viongozi wakuu M/kiti na Katibu wake ndani ya chama. Mwanaripota wetu ndani ya mtaa wa UFIPA yaliopo makao makuu ya chama anadai kumekuwepo na vikao vya Mara kwa Mara baada tu kusigana na Mzalendo zito zuberi kabwe.

PICHA: Aibu,aibu,aibu hii ndio halisi halisi jimbo la lushoto,salamu kwa CCM


Mbatia ashinda tena NCCR, mizengwe yatawala mkutano

Uchaguzi Mkuu wa nane wa Chama cha NCCR-Mageuzi, umemchagua tena James Mbatia kuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa kipindi kingine cha miaka mitano ijayo huku mizengwe ikitawala katika uchaguzi huo. Katika uchaguzi huo ulioanza juzi, idadi kubwa ya wajumbe walikuwa na mkakati wa kumng’oa Katibu Mkuu, Samwel Ruhuza aliyekuwa akitetea nafasi yake, Mosena Nyambabe na Rehema Sam waliokuwa wakiitaka nafasi hiyo.

Dr. Slaa: Baraza jipya limechoka kabla halijaanza kazi

Katibu mkuu wa Chadema Dr. Willbrod Slaa amesema kwamba baraza jipya la mawaziri lililoteuliwa na kutangazwa jana na katibu mkuu kiongozi limechoka kabla halijaanza kufanya kazi. Aidha Dr. Slaa amesema kuwa uteuzi wa Mwigulu Nchemba kama naibu waziri wa fedha (sera) ni mkakati wa CCM kujichotea fedha za uchaguzi mkuu ujao hivyo tutarajie EPA nyingine.

Mambo matatu yaitesa CCM

MBIO za kusaka urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), na uteuzi wa nafasi nne za mawaziri, vinaelezwa kukibomoa chama hicho, Tanzania Daima limedokezwa. Mbali na mambo hayo, mchakato wa uundwaji wa katiba mpya ambayo rasimu ya pili imetoka hivi karibuni na kuingizwa kwa serikali tatu, umeonekana kukiathiri zaidi chama hicho kinachotaka uwepo wa serikali mbili. Tayari viongozi wa CCM wameshaanza maandalizi ya kukutana na wabunge, wawakilishi na wabunge wa Bunge la Katiba watakaochaguliwa, kwa lengo la kuweka msimamo wa kutopitisha serikali tatu wakati wa majadiliano.

MHE EZEKIEL MAIGE - UFAFANUZI WANGU KUHUSU TUHUMA KUWA NINAMILIKI NYUMBA YA KIFAHARI

Wapendwa,


Salaam za pilika za maisha?

Nimeona ni vema nikawafafanulia, kwa baadhi ambao hamkufuatilia kipindi cha Medani za Siasa kilichorushwa na Star TV jana mchana.

Nimeona nifanye hivyo baada ya upotoshaji wa kitoto, uliojaa roho mbaya na chuki za makusudi uliofanywa na mtu anayejiita Kiroba kwenye mtandao wa Jamii forums.

Star TV hufaya kipindi cha Medani za Siasa kwa wanasiasa mbalimbali kila wakati. Katika vipindi vyao, huongea na mwanasiasa wanayemchagua kwa wakati huo na humuuliza mambo mengi yanayomuhusu na mambo yake ya siasa.

Chuki zaanza ndani ya CCM, Sinyanga, Monduli, Mgeja, Lowasa

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Mkoa wa Shinyanga, Hamisi Mgeja akizungumza na wanachama. Picha na Mwandishi Wetu 
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Mkoa wa Shinyanga, Hamisi Mgeja ameonya baadhi ya viongozi wa chama hicho kuwajengea chuki wanachama kadhaa na viongozi kwa madai wako karibu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa. Hatua ya Mgeja imekuja ikiwa ni siku chache baada ya Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Geita, Joseph Kasheku ‘Msukuma’ kumkana na kumshutumu, Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM, Mgana Msindai kuwa anawalazimisha kuwa nyuma ya Lowassa wakati sivyo ilivyo.

Sunday, 19 January 2014

Taarifa ya Mbunge, Cyril Chami kuhusu ukurasa ulioanzishwa kwa jina lake Facebook

Picture
Naitwa Cyril August Chami (PhD) Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini na Mjumbe wa NEC-CCM kupitia Wilaya ya Moshi Vijijini.


Nimesikitishwa na kufadhaishwa sana na mtu au watu waliotengeneza akaunti kwa jina langu kwenye  Mtandao wa Kijamii wa Facebook na kujifanya yeye au wao ndio mimi.

Wamepachika hata picha zangu zinazopatikana kirahisi kwa sababu ya majukumu ambayo nimeshawahi kuwa nayo kama Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, na Waziri wa 
Viwanda na Biashara.