
Wakuu,mimi huwa nakereka sana ninapohudhuria mikutano ya baadhi ya wabunge wa CHADEMA.
Nianze hivi,
Ukienda jijini mbeya karibu eneo kubwa la barabara za mitaa zimepigwa lami,sasa BWANA JOSEPH MBILINYI anajitapa kuwa yeye ndo aliyeleta hiyo lami kana kwamba alitoa pesa yake mfukoni. Jamani,hizi barabara ni mpango wa uboreshaji wa majiji na bado ilikuwa ni utekelezaji wa ilani ya chama kilichopo madarakani.
Nenda MWANZA,ARUSHA, DAR kuna mchakato kama huo.
Lakini tukiondoa mchakato huo wa majiji ukienda DODOMA barabara zipo safi pana CHADEMA pale?
Nenda SONGEA kuelekea MBINGA na NAMTUMBO kuna lami nayo ni ya CHADEMA?
Wakuu najua yapo maeneo mengine mnayafahamu yana maendeleo ya barabara na hao CHADEMA hawapo.Kwa nini wanawadanganya wananchi kwa hili?
Kuna miradi ya maji MANISPAA ya IRINGA inayotekelezwa na serikali lakini BWANA PETER MSIGWA anapita mitaani na kujigamba kuwa ndo aliyeileta hivi ni kwa nini mpo hivyo?
Msitake kutuaminisha kuwa SIASA ni uongo hebu jaribu kuwa wakweli jamani
Na K wa JF
No comments:
Post a Comment
Tuandikie maoni yako kuhusu habari hii
Asante kwa Mchango wako