
Wanaukumbi.
Chama chochote makini lengo lake ni kutwaa dola, kutwaa dola kuna kuja baada kuwaeleza wananchi nini dhumuni lenu kama chama cha siasa, wananchi wanataka kufahamu mtawafanyia nini kama wakiwachagua kuingia Ikulu, kwenye masuala muhimu Afya, Elimu, Kilimo, Uchumi wa Nchi, Mahusiano ya Kimataifa, Ajira kwa Vijana, tatizo la watanzania siyo Chopa wala maandamano.
Chadema wamekuwa kila siku wanakuja na operesheni za majina tofauti tofauti lakini hakuna tija yeyote kwa wananchi zaidi ya fujo, hata siku moja hauwezi kumskia Lema au Sugu wakiongelea masuala ya kiuchumi, biashara au mipango ya ajiea kwa vijana, hizi operesheni za Chadema hazina tofauti na matamasha ya Fiesta, watu wengi wanaojitokeza viwanjani hawaji kusikiliza sera wanakuja kuangalia Chopa kisha wanarudi majumbani.
Chadema hamuwezi kuchukuwa nchi kwa ushabiki wa Chopa na Maandamano watanzania hawana shida na Chopa.
Na R wa JF
No comments:
Post a Comment
Tuandikie maoni yako kuhusu habari hii
Asante kwa Mchango wako