Friday, 17 January 2014

Chama cha Kilaghai Tanzania...

CHADEMA ni chama kinachoendeshwa kwa misingi ya ulaghai. Chama kama hiki mtu yeyote atakayetaka kukiunga mkono kwa hoja anajikuta anakwazika.  Hii imesababisha CHADEMA kuungwa mkono zaidi na makundi mawili ya watanzania: 


1. wale ambao ni bendera fuata upepo. 
2. wale wenye malengo ya kupanda haraka na kwa urahisi kwenye arena za kisiasa za kitaifa.
Nitayachambua makundi haya mawili kama ifuatavyo:

1. Wale ambao ni bendera fuata upepo. Katika kundi hili kuna watu wa aina tatu:

i) Wale ambao wamedanganyika na propaganda kuwa chadema ni chama cha kikabila au cha kikanda na kwa vile wao wanatoka kwenye kanda hizo basi wanajisikia ukaribu zaidi na chadema. Hapa utaona kuwa propaganda za kukichafua chama kuwa ni cha kikabila au cha kikanda kimeweza kuwaongezea chadema nguvu katika maeneo inayoshutumiwa kuyapendelea.

ii)Wale ambao wamelaghaika na propaganda za kuwa chadema ni chama cha udini. Kuna waumini wengi wameviunga mkono vyama vya chadema na CUF kwa sababu tu wamekuwa wakisikia kuwa vyama hivyo vinashabiiana na dini zao. Hawa ni bendera fuata upepo ambao hawachuji ukweli wa taarifa na hawajiulizi chama kinaweza kuwanufaishi vipi kama waumini wa dini husika. 

iii)Kundi la tatu katika bendera fuata upepo ni vijana ambao wanaona kuwa chadema ni kama fashion. Ukikaa nao chini vijana hawa kuwauliza kwanini wanaiunga mkono chadema hawana lolote la kuongea. Mfano wa watu waliomo kwenye kundi hili ni members wa jamiiforums ambao hurusha matusi kwa kila mtu anayehoji jambo juu ya chadema.

Makundi haya matatu ya bendera fuata upepo huwa ni rahisi sana kuvunjwa moyo na kukikimbia chama mara tu upepo utakapoelekea upande tofauti. Kwa mfano, iwapo chadema itafanya jitihada za kuhakikisha jamii inajua ukweli kuwa siyo chama cha ukanda wala ukabila, basi makundi haya mawili i) na ii) yatatoweka. 
Vilevile iwapo chadema itasambaza elimu ya uraia na kuwawezesha wananchi kuchagua vyama vyama vya kuviunga mkono kwa hoja, basi makundi yote iii),ii) na i) itayapoteza. 
Hizi ni changamoto zinazohitaji political calculations kudeal nazo.

2. Wale wenye malengo ya kupanda haraka na kwa urahisi kwenye arena za kisiasa za kitaifa:
Katika kundi hili wamo wanasiasa kama Dr. Wilbroad Slaa na Shibuda. Misingi ya wanasiasa wa aina hii kuhama kutoka kwenye chama kimoja mpaka kingine ni kuhakikisha tu kuwa wanaendelea kuwepo kwenye shughuli za kisiasa katika nafasi za uongozi. Hawana ugomvi wa kiitikadi na CCM.

Kimsingi hawa ni watu ambao iwapo leo hii CCM itawahakikishia kuwa watapata fursa ya kuwa viongozi wa juu, basi wako tayari kujiunga nayo. Wamejitoa CCM kwa sababu tu walinyimwa fursa ya kuwa viongozi katika ngazi walizogombea. Iwapo chadema itawanyima fursa ya kuwa viongozi, wataikimbia pia. 
Mfano mzuri umeonekana hivi karibuni Lushoto ambaye kijana mpya katika siasa Deogratius Kisandu aliikimbia chadema kwa kukosa fursa za uongozi ambapo kimsingi alijiunga chadema kwa kuamini kuwa fursa hizo atazipata kwa urahisi zaidi ndani ya chama hicho.

CHADEMA imekosa uungwaji mkono katika misingi ya itikadi. Hii imesababishwa na ukweli kwamba cHADEMA imechukua itikadi zilezile za CCM, TANU na ASP na kushindwa kuwapa wananchi chaguo jipya. Zaidi ya hayo, hata kwenye ilani za uchaguzi za chadema hakuna offer tofauti na zile ambazo wananchi wanapewa na CCM. Kuthibitisha hili, chadema imepata wakati mgumu sana kupokelewa katika maeneo ambayo kuna chama kingine cha upinzani kilichojijenga kama Zanzibar. Iwapo chadema wangekuwa na itikadi au sera mpya ambazo utekelezaji wake unaelezeka, isingekuwa vigumu kupata wafuasi katika maeneo hayo. 

Kwa vile CCM imeshapewa fursa ya kutawala, mapungufu yake yameonekana. Jukumu la chadema kwenye hili linatakiwa ni kuja na mkakati unaoelezea kwa undani ni vipi watafanya tofauti na CCM. Badala yake, kazi pekee inayofanywa na chadema ni kuainisha matatizo na kuyahubiri majukwaani bila kuelezea iwapo wana mkakati wowote mpya ili wananchi waupime. Hii inasababisha hata wasomi wanapovifananisha hivi vyama wanakosa zile tofauti za kuzijadili na mwishowe hujadili tabia za viongozi vya vyama na utendaji wao badala ya kujadili sera zake na itikadi.

Ulaghai wa CHADEMA ni sababu nyingine iliyofanya chama hiki kupoteza wafuasi makini. Mtu yeyote atakayejaribu kuichunguza chadema kidogo tu atagundua kuna mambo mengi yasiyofaa yanayofanywa na viongozi wake. Viongozi hawa hufanya hivi kujinufaisha wao wenyewe na familia zao. Kwa vile umaarufu wa chadema umetokana na uhubiri wa ufisadi, uwepo wa ufisadi ndani ya chadema umewavunja sana moyo wananchi walioamini kuwa wamepata tumaini jipya. Wale wanaoishabikia chadema kwa kufuata upepo wanapojua ulaghai huu, huvunjwa moyo na kuikimbia. Mfano wa hili ni kijana Mtela Mwampamba ambaye aliamini kuwa chadema ni tumaini jipya mpaka pale alipojionea mwenyewe kwa macho yake uhalisia wa mambo ndani ya chama hicho.

Hapa nitaainisha baadhi ya mambo yanayoiondoa CHADEMA usoni na moyoni mwa watanzania wanaotaka chama kinachopinga ufisadi.
1. Mmiliki wa jengo lililopangishwa na CHADEMA Kinondoni kama ofisi za makao makuu na bei ya pango kwa mwezi vimefanywa siri. Mara kadhaa swali hili limeibuliwa lakini hakuna jibu lililoweza kutolewa na uongozi wa CHADEMA.

2. Wanachama walioomba fursa ya kushiriki tenda ya kununua magari ya chama wamenyimwa fursa hiyo na hatimaye tenda hiyo imetolewa kwa usiri mkubwa. Chris Lukosi amekuwa akishutumiwa kuwa sababu ya kujitoa kwake CHADEMA ni kunyimwa tenda hii, lakini pale wadau walipohoji baada ya Lukosi kunyimwa tenda hiyo ni nani amepewa na kwa vigezo vipi?, kinaibuka kigugumizi.

3. Swala la Katibu Mkuu wa chama kujikopesha mamilioni ya shilingi zilizochangwa na walalahoi kwa ajili ya shughuli za chama. Ikumbukwe kuwa watu waliochangia M4C walifanya hivyo kwa vile waliamini kuwa michango yao itakiwezesha chama kujiimarisha. Taarifa kuwa pesa zimetumika kifisadi zimewavunja watu moyo.

4. Taarifa za Josephine Mushumbusi kulipwa mamilioni ya shilingi za chama kwa kazi anayoiita ya kujitolea. Wadau walihoji kuwa na wao wangependa kujitolea kwenye shughuli za chama ili walipwe hayo mamilioni. Ilidhihirika kuwa Josephine alipata fursa hiyo kwa upendeleo.

5. Pesa za ruzuku zimekuwa zikiishia Makao Makuu. Watendaji wa chama mawilayani wamekuwa wakifanya kazi bila nyenzo. Hii ilisababisha mpaka kukawa na mtafaruku huko Mpanda kwa kukosa ofisi ya wilaya ambayo kimsingi ni jukumu la chama makao makuu kuhakikisha chama kina ofisi za wilaya. Ikumbukwe pia kuwa matumizi haya mabaya ya fedha yalikuwa sababu ya mvutano wa kisiasa kati ya marehemu Chacha Wangwe na kiongozi Mkuu wa Chama.

6. Kumekuwa na taarifa za matumizi mabaya ya pesa za Sabodo jambo ambalo limeelezewa kuwa sababu ya kumfanya Sabado kuahirisha ahadi yake ya kuijengea CHADEMA ofisi za makao makuu na chuo cha siasa.

7. Katibu Mkuu wa CHADEMA ni miongoni mwa washutumiwa wa ufisadi wa mamilioni ya pesa za mradi wa maji wa Karatu.

8. Viti Maalum vya ubunge vimetolewa kwa upendeleo ambapo akinamama waliojitolea kukijenga chama wameachwa pembeni na nafasi hizo kupewa akinamama walio karibu na viongozi wa juu wa chama. Hapa ikumbukwe kuwa mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) wa Taifa alishinda nafasi ya uchaguzi wa viti maalum, lakini akatolewa kwa kuambiwa kuwa hajakidhi vigezo vya kuwa mbunge ingawa amewaongoza wanawake wenzake kwa muda mrefu ndani ya chadema. Wakati huohuo mwanamama anayeishi Marekani, Leticia Nyerere amepewa Ubunge wa viti maalum kutokana na "kufahamiana" na mwenyekiti wa chama. Hili limewavunja moyo wengi walioanza kuiamini chadema.

9. Vijana kama Kafulila walioonekana kuwa na ari ya mabadiliko ndani ya chama wamekuwa wakinyimwa nafasi ya kugombea uongozi kinyume na katiba.

10. CHADEMA kukanusha kauli ya Nape kuwa wanapewa msaada na chama cha siasa cha Ujerumani, baadae ikadhihirika kuwa ni kweli wanapokea msaada huo. Hii imedhihirisha kuwa CHADEMA sio wawazi katika utendaji wao. Wadau wanajiuliza chama hicho cha siasa kinataka nini Tanzania mpaka kikipinge chama kilichoasisiwa na wapigania Uhuru na kutaka chadema iingie madarakani? Ikumbukwe kuwa muasisi wa CHADEMA Mzee Mtei, alikataa kushiriki harakati za kupigania uhuru na pia alikataa kujitolea kuijenga nchi baada ya Uhuru.

11. Hesabu za pesa zinazochangwa na walalahoi kwa ajili ya M4C imekuwa ni jambo la siri kubwa ndani ya CHADEMA.

Na Z , JF

No comments:

Post a Comment

Tuandikie maoni yako kuhusu habari hii
Asante kwa Mchango wako