UCHAGUZI KATA YA NYASURA WILAYA YA BUNDA HATARINI KUTOKUFANYIKA.
Uchaguzi wa kata ya Nyasura wilaya ya Bunda hatarini kutokufanyika.
Kwa nini?!
2. Vikao viwili vya ulinzi na usalama(mkoa na wilaya) mkoa chini ya John Tuppa na kuhudhuriwa na Mh Wassira, na wilaya chini ya mkuu wa Wilaya Bwana Mirumbe ambaye baba yake alikuwa mwanamtandao na mpiga kampeni wa JK 2005. Vikao hivyo vimekuwa na maazimio ya kuharibu uchaguzi ikiwezekana kuchoma nyumba za nyasi siku ya kesho ili ionekane kuwa Nyasura hakuja tulia na hivyo kuahirisha uchaguzi kama jinsi ilivyotokea kwenye bomu la Soweto kule Arusha.
3. Wamefikia uwamuzi wa kusafirisha kikosi cha wanajeshi ambao wataingia kesho usiku kwa ajili ya kuwadhibiti vijana wa chadema wa RB ambao wameapa kutokukubali hujma zozote dhidi ya uchaguzi wa siku ya jumapili.
4. Wamewalipa mabalozi shilingi 5000 kila mmoja kwenye kata nzima ya Nyasura ili watumike kuwahamasisha watu wapigie kura ccm na wale ambao wataonekana hawataiunga mkono ccm wapeleke majina yao ili ufanyike utaratibu wa kununua viparata vyao vya kupigia kura. Mabalozi hao wameahidiwa kununuliwa mabati kama uchaguzi utafanyika na ccm kushinda.
Kiujumla ccm hali yao ni mbaya sana na hata uzinduzi wao wa kampeni ulifanyika kwa kuchelewa juzi baada ya Mh Wassira kushindwa kuzindua kampeni mara mbili.
Mgombea udiwani wa chadema anaitwa Julius Magambo Wassira mtoto wa kaka wa Mheshimiwa Wassira. Mtakumbuka kuwa mara kadhaa Wassira amewakana watoto wa ndugu zake waliojiunga CHADEMA.
Na Y. N wa JF
No comments:
Post a Comment
Tuandikie maoni yako kuhusu habari hii
Asante kwa Mchango wako