MBUNGE wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumjeruhi kada wa Chama Cha Mapunduzi (CCM) kwa kitu kitu kizito. Mchungaji Msigwa alifikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa, Godfrey Isaya jana na kusomewa shitaka moja la kujeruhi. Akisoma shitaka hilo Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Elizabeth Swai alidai Mchungaji Msigwa alitenda kosa hilo Febrauri 5, 2014 katika kijiji cha Nduli mjini Iringa.
Alidai Mchungaji Msigwa anashitakiwa kwa kumjeruhi Salum Kahita.
Alidai Mchungaji Msigwa anashitakiwa kwa kumjeruhi Salum Kahita.
Mchungaji Msigwa anayetetewa na wakili Lwezaula Kaijage alikana kosa hilo na hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 18 mwaka huu. Mbunge huyo yupo nje kwa dhamana.
Jeshi la Polisi pia limewapandisha kizimbani Meshack Chonanga (22) na Paulo Mapunda wote wakazi wa Kijiji cha Nduli mjini Iringa kwa madai ya kumjeruhi Alex Mpiluka ambaye ni mwanachama wa Chadema wakati wa kampeni hizo.
Kukamatwa kwa mbunge huyo kulitokana na vurugu kubwa zilizoibuka juzi katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Nduli, Manispaa ya Iringa.
Katika kampeni hizo inadaiwa wafuasi wa Chadema waliwashambuliwa wafuasi wa CCM kwa mawe na nondo ambako kijana mmoja, Salum Kaita alijeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa kwa matibabu.
Mashududa wa tukio hilo walisema kuwa wakati vijana wa CCM wakiwa katika mkutano wa kampeni ghafla walivamiwa na wafuasi wa Chadema waliowashambulia kwa mawe na nondo.
NA RAYMOND MINJA, IRINGA
No comments:
Post a Comment
Tuandikie maoni yako kuhusu habari hii
Asante kwa Mchango wako