“Mungu amempa uwezo akisimama watu humfuata nyuma katika kusaidia wanyonge, yeye ana nguvu za Mungu, nadhani hiyo ndiyo inamletea taabu. Sasa mimi niulize kuna kamati za maadili sawa, tangu mwaka 1993 ameanza harambee leo wanasema ameanza kampeni?” alihoji Nangole. Alisema Lowassa amekuwa akisaidia kila pembe ya nchi katika nyumba za ibada na hafanyi kampeni, kwani hao wanaosaidiwa siyo wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM.
Amshambulia Malecela - Alisema anamheshimu sana Makamu Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho, John Malecela na alidhani angetumia busara zake kumsaidia Rais Kikwete ili kukabiliana na matatizo ya kijamii kuliko kuibua suala la fulana za kuashiria Lowassa ameanza kampeni.
“Tuna matatizo ya ajira, elimu, afya, ajali, rais anahangaika usiku na mchana, ningedhani huyu mzee mwenye umri mkubwa ameongoza nchi kama Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Makamu Mwenyekiti wa CCM, angemshauri Rais kwani tuna matatizo mengi kuliko fulana. Mimi nadhani busara zake zingesaidia taifa kuliko fulana ambazo hata wanamichezo wanapewa. Nimesikitika sana,” alisema Nangole.
Nangole amekuwa mwenyekiti wa tatu wa CCM mkoa kujitokeza hadharani na kutoa matamshi ya kutetea kinachoelezwa kama mienendo ya Lowassa.
Wengine ni Khamis Mgeja wa Shinyanga na Mgana Msindai wa Singida wanaoungana na wabunge, John Komba wa Mbinga Magharibi na Beatrice Shellukindo wa Jimbo la Kilindi.
Lowassa asiwe na hofu - Kwa upande wake ole Kuney alisema anashangaa watu wanaomshambulia Lowassa bila sababu za msingi hasa kuhusiana na mbio za urais ambazo hata hajatangaza.
“Mbona watu wengi wanasema wanataka kugombea na wanajulikana, mbona hawasemwi. Tunamwomba Lowassa asiwe na hofu awapuuze hawa watu, wanatapatapa kama wafamaji,” alisema Ole Kuney.
Alisema lazima ijulikane Lowassa ana watu, ana marafiki wa kila aina, kwa hiyo akizunguka na wajasiriamali hakuna tatizo.
“Mungu amempa uwezo akisimama watu humfuata nyuma katika kusaidia wanyonge, yeye ana nguvu za Mungu, nadhani hiyo ndiyo inamletea taabu. Sasa mimi niulize kuna kamati za maadili sawa, tangu mwaka 1993 ameanza harambee leo wanasema ameanza kampeni?” alihoji Nangole.
Alisema Lowassa amekuwa akisaidia kila pembeya nchi katika nyumba za ibada na hafanyi kampeni, kwani hao wanaosaidiwa siyo wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM.
Amshambulia Malecela - Alisema anamheshimu sana Makamu Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho, John Malecela na alidhani angetumia busara zake kumsaidia Rais Kikwete ili kukabiliana na matatizo ya kijamii kuliko kuibua suala la fulana za kuashiria Lowassa ameanza kampeni.
“Tuna matatizo ya ajira, elimu, afya, ajali, rais anahangaika usiku na mchana, ningedhani huyu mzee mwenye umri mkubwa ameongoza nchi kama Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Makamu Mwenyekiti wa CCM, angemshauri Rais kwani tuna matatizo mengi kuliko fulana. Mimi nadhani busara zake zingesaidia taifa kuliko fulana ambazo hata wanamichezo wanapewa. Nimesikitika sana,” alisema Nangole.
Nangole amekuwa mwenyekiti wa tatu wa CCM mkoa kujitokeza hadharani na kutoa matamshi ya kutetea kinachoelezwa kama mienendo ya Lowassa.
Wengine ni Khamis Mgeja wa Shinyanga na Mgana Msindai wa Singida wanaoungana na wabunge, John Komba wa Mbinga Magharibi naBeatrice Shellukindo wa Jimbo la Kilindi.
Lowassa asiwe na hofu - Kwa upande wake ole Kuney alisema anashangaa watu wanaomshambulia Lowassa bila sababu za msingi hasa kuhusiana na mbio za urais ambazo hata hajatangaza.
“Mbona watu wengi wanasema wanataka kugombea na wanajulikana, mbona hawasemwi. Tunamwomba Lowassa asiwe na hofu awapuuze hawa watu, wanatapatapa kama wafamaji,” alisema Ole Kuney.
Alisema lazima ijulikane Lowassa ana watu, ana marafiki wa kila aina, kwa hiyo akizunguka na wajasiriamali hakuna tatizo.
Na Mussa Juma, Mwananchi
No comments:
Post a Comment
Tuandikie maoni yako kuhusu habari hii
Asante kwa Mchango wako