
Akiongea muda huu katika kipindi cha ITV cha "dakika 45" waziri kivuli wa mambo ya ndani,mh.Vicent Nyerere (pichani) ametoa kali kwa kusema kutokana na ugumu wa maisha unaowakabili polisi wetu leo hii ukamtumia polisi ujumbe wa "tafadhali nipigie",yeye atakujibu kwa ujumbe wa "tafadhali niongezee salio"!
Mh.Nyerere anasema inafikia hatua polisi anamsimamisha mwendesha baiskeli na kumuhoji kwanini baiskeki yake haina medigadi.Kali zaidi amesema katika kutafuta hela polisi wanamsimamisha mtu mwenye gari la kubeba abiria wanne kwa mfano na kumuhoji ni kwanini yuko peke yake!Hizo zote amedai ni mbinu za polisu kubambikizia watu(madereva) makosa ili wapate fedha.
Mh.Nyerere ameenda mbali kwa kusema RPC anawapa kazi vijana wake za kulisha familia.Yaani anawapangia wewe utalisha familia yangu akimanisha askari hao watafute fedha wakiwa kazini na kumpelekea yeye(RPC).
Ilifika hatua mtangazaji akamuonya kuwa anaongea na chombo cha habari ila yeye akamjibu kuwa ana ushahidi wa anayoyasema.
Mbali na hilo,mh.Nyerere amesema hata viatu vya polisi siku hizi havifanani kwani wanatafuta mtumbani.Yaani kila polisi anajitafutia sare za viatu vyake.
Mh.Nyerere kaongea mengi ya kusikitisha na ameweka wazi kuwa mke wake ni polisi ila haishi maisha magumu kwasababu tu ni mke wa mbunge.
MY TAKE:Kwa matamshi haya,tusubiri kusikia mh. Nyerere amekamatwa au ameagizwa ajisalimishe polisi kutoa maelezo kuhusu kauli zake hizi.
Tusubiri tuone.
Na S.S wa JF
No comments:
Post a Comment
Tuandikie maoni yako kuhusu habari hii
Asante kwa Mchango wako