
Mgombea wa nafasi ya uwakilishi jimbo la kiembe samaki Bwana Abdull Malik Haji akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Chama Taif Prf.Lipumba baada ya kukabidhiwa manufesto ya chama.[/captio0n]Chama cha Wananchi CUF kimesema hakiutokuwa tayari kudhulumiwa na kufanyiwa hujuma kama zilizofanywa katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Bububu.
Kauli hio imesemwa leo na Mkurugenzi wa haki za Binadamu,habari,uenezi na mahusiano ya umma,Mh Salim Bimani wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo viwanja vya bustanini Jimbo la Kiembe Samaki.
Amesema ipo kila sababu kwa serikali ya mapinduzi Zanzibar kuhakikisha wanayalinda maridhiano ili kuepusha maafa ambayo sivyema kutokea tena ndani ya visiwa hivi.
Nae Naibu katibu mkuu wa Chama hicho Mh,Hamad Massoud Hamad ameleza kwamba maamuzi ya kiburi yaliofanywa na CCM yamekuwa yakiwaathiri sana wananchi wa Zanzibar husani katika suala zima la maendeleo.
‘’Nitawashangaa sana wananchi wakiembe samaki kuona bado munaendeleza kumchagua mgombea wa CCM wasioitakia mema Nchi hii’’alisema Bwana Hamad Massoud.
Alitolea mfano wa Chama cha wananchi CUF mara kadhaa kimekuwa kikiwafukuza baadhi ya watu uanachama akiwemo Binaila Jidawi na Hamad Rashid lakini hakukuwahi kuitishwa uchaguzi mdogo lakini jimbo la kiembe samaki umeitishwa kwa sababu tu Mansour alikuwa akiwatakia mema wazanzibar.
Nae mgeni rasmi katika mkutano huo Mwenyekiti wa Chama Taifa Prf,Ibrahim Harouna Lipumba aliwataka Wananchi kukumbuka uzalendo wa aliekuwa mtoto wa mwana mapinduzi na mwakilishi wa Jimbo hilo Mansour Yussuf Himid jinsi alivokuwa mstari wa mbele kuitetea Zanzibar yenye maslahi yake.
‘’Nawaombeni wananchi wa Kiembe samaki mchagueni mgombea wa CUF ili akayaendeleze aliyokuwa akiyatetea Mansour ndani ya Baraza la wawakilishi’’aliesema Lipumba.
Pamoja na hayo amewaasa wananchi wa Jimbo hilo kuhakikisha wanaleta mabadiliko katika safu ya uwongozi kwa kumchagua Mwakilishi makini Bwana Abdull Maliki kutoka chama cha wananchi CUF ambacho ndio chama pekee chenye msimamo wa kuidai Zanzibar huru.
Kwa upande Wake mgombea huyo wa nafasi ya uwakilishi Bwana Abdull Malik amewaasa wananchi wa Jimbo hilo kuhakikisha wananchamgua na kuwa mwakilishi wa Jimbo la kiembe samaki ili akaendeleze harakati za kudai Zanzibar huru.
‘’Anaeleta masihara na Nchi huyo hana uchungu wa Nchi ni bora kuachana nae’’alisema mgombea huyo.
Licha ya hayo aliwaeleza wananchi wa Jimbo hilo kujua kuwa kazi iliopo kwa sasa ni moja tu kuhakikisha wanampa kura kwa wingi ili aingie barazani.
Aidha amewaahidi wananchi wa Jimbo hilo kuyatetea yale yote aliyokuwa akiyadai Mansour juu ya maslahi ya Wananchi wa Zanzibar dhidi ya Nchi yao.
Uchaguzi mdogo wa kiembe samaki utafanyika siku ya atarehe 2/2/2014 kutokana na aliekuwa Mwakilishi wa Jimbo hilo kufukuzwa uanachama ndani ya CCM.
No comments:
Post a Comment
Tuandikie maoni yako kuhusu habari hii
Asante kwa Mchango wako