Saturday, 18 January 2014

Mbunge Temeke akabidhi madawati 500 shule za msingi

Mbunge wa jimbo la Temeke, Abass Mtemvu (pichani), amekabidhi madawati 500 kwa ajili ya shule za msingi. Akizungumza wakati akikabidhi kwa uongozi milioni 67.5/- ambao  yametengenezwa na Chuo cha Ufundi (Veta) Chang'ombe kutokana na fedha za mfuko wa jimbo hilo.Alisema kukamilika kwa idadi hiyo ni  mwanzo wa kuondokana na tatizo la ukosefu wa madawati kwa shule za msingi na sekondari ndani ya eneo lake.
Mtemvu, aliongeza kwamba yeye kwa kushirikiana na madiwani wameandaa mkakati wa kuchangisha pesa ili shule zote ziwe na madawati ya kutosha
Afisa elimu wa msingi wa Manispaaya Temeke, Honorina Mumba, alimshukuru Mbunge huyo kwa kujikita katika elimu kwa kuhakikisha matatizo mbalimbali yanapatiwa ufumbuzi.
Alisema madawati hayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa kuziba pengo lilopo la ukosefu wa madawati kwa shule za msingi na wanatarajia kwa nguvu zake pamoja na madiwani suala hilo litafikia mwisho. 
NA MOSHI LUSONZO, NIPASHE

No comments:

Post a Comment

Tuandikie maoni yako kuhusu habari hii
Asante kwa Mchango wako