Monday, 20 January 2014

PICHA: Aibu,aibu,aibu hii ndio halisi halisi jimbo la lushoto,salamu kwa CCM




Mbunge wa jimbo la Lushoto Mkoani Tanga Ndugu Henry Daffa Shekifu amepata salamu za 2014 kuelekea 2015,wananchi wanazidi kuikataa CCM,wananchi wa Lushoto wananza kukataa kuburuzwa. Mwenye suti ya Dark Blue(aliyekaa) kulia ni Mbunge wa jimbo la Lushoto akitafakari hatma yake ya kisiasa kuelekea 2015,hali ni mbaya.Aliyevaa hijabu ni Katibu Kata.
Hii ilikuwa kwenye mkutano wa Hadhara ambao ulipaswa kufanyika kata ya Lushoto,kijiji cha Magamba karibu na Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa Memorial University(SEKOMU). Kazi ya CHADEMA ni msingi inaendelea kwa kasi jimbo la Lushoto, magamba wanazidi kusambaratika, walichobakiza ni ubabe tu!!!!!Itajulikana 2015.


Na M.G, JF

No comments:

Post a Comment

Tuandikie maoni yako kuhusu habari hii
Asante kwa Mchango wako