Friday, 24 January 2014

Mamilioni ya Lowassa yaingia CHADEMA?

Katika kile kinachoonekana kujihakikishia Urais 2015 aliyewahi kuwa waziri mkuu (sio waziri mkuu mstaafu kwani uwaziri sio nafasi ya kuajiriwa na kisha kustaafu) ndugu Lowasa ameanza ama anaendeleza kazi ya kuwamgia mamilioni viongoz wakuu wa chadema katika kumsafishia njia. Najua suala hili litashtusha wengi lakini ndio uhalisia kwani tangia mwaka 2010 viongozi wa kitaifa wa CHADEMA wamebakia kuwaandama viongozi wengine wa CCM huku wakifumbia madudu na uchafu anaoendelea kuufanya Lowasa kama kwamba hawaoni hadi hatua ya wanachama na wapenzi kuanza kuhoji kwa nn Lowasa hazungumziwi? ambapo majibu rahisi na yasiyo na mshiko kutoka kwa viongozi wa chama ni kwamba Lowasa kwa kuwa atapishwa na CCM mwaka 2015 kugombea urais sio sawa kumzungumzia kwa sasa kwani kutampa mwanya wa kujisafisha katika kashfa zake na hivo kukosa hoja za kumchafua kwa wananchi kama ilivyo kawaida ya siasa za Tanzania ili upendwe unatengeza fitina mwenzio achukiwe.  ukweli ni kwamba Lowasa amekuwa akiwapa mamilioni viongozi hao ili kuwadhoofisha wapinzani wake na hatimaye kujihakikishia kupitishwa na chama chake kugombea uraisi.

Lowasa na Zitto kabwe.
kuna taarifa za chinichini kuwa kufukuzwa kwa Zitto kabwe pia kuna mkono wa Lowasa amabaye ni mmoja wa vigogo walioficha pesa nje na hivyo kama njia ya kudhoofisha mjadala wa pesa hizo kurudishwa ni kumuudhofisha mtoa mada na hivyo Lowasa alimwaga pesa zilizotumika kushawishi wajumbe wa kamati kuu ya CHADEMA kumuondoa Zitto na kufanikisha mikutano nchi nzima ya kuweka upepo sawa kujinuru na kifo cha mpasuko wa chama.

CHADEMA WAANZA KUMPIGIA KAMPENI LOWASA.
Hivi karibuni licha ya kutokuzungumzia rushwa za kutisha ambazo lowasa anazitoa, viongozi wa chadema wameanza kumpigia debe kiaina lowasa kwa kuueleza umma kwamba anachotoa lowasa ni misaada na isiwafanye wamuunge mkono. Chadema wanasema wananchi wamuunge mkono lowasa kama ataamua kugombea kupitia chama kingine ambacho si CCM na kwa maana hii Chadema wako tayari kumpokea mtu huyu ambaye miaka mitatu minne iliyopita walimandama kwa kumwita FISADI wa Richmond na mengine mengi. Ama kweli PESA SABUNI YA ROHO!!!!!!
katika operesheni ya chadema ya sasa Lowasa ananadiwa LIVE na ukitaka ushahidi wa wazi rejea gazeti la leo la mwananchi 24/01/2014 "CHADEMA: BODABODA ACHANENI NA LOWASSA" Ambapo chadema kinadai "MUNAWEZA KUMUUNGA MKONO KAMA AKIACHANA NA CCM NA KUAMUA KWENDA CHAMA KINGINE".
Hakuna kama pesa, hakuna kama rushwa, tuna safari ndefu sana kupata upinzani wa kweli na kupata viongozi sahihi. ninchojiuliza ni Haya mamilioni yanayopelekwa chadema na sehemu nyingine yatarudishwaje? na hizi hasira na usongo wa uraisi anaoukimbilia lowasa akipita nini kitajr?


No comments:

Post a Comment

Tuandikie maoni yako kuhusu habari hii
Asante kwa Mchango wako