UMOJA wa viongozi wa wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania umempendekeza Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Januari Makamba, kuwa ndio anayefaa kuwania nafasi ya Urais katika uchaguzi ujao wa mwaka 2015 kwakuwa hajawai kuhusishwa na kashfa za rushwa na ufisadi . Umoja huo unakusudia kutembea nchi nzima kwajili ya kushawishi wananchi kumchagua Makamba katika kinyanganyiro cha na nafasi ya urais katika uchaguzi ujao kwakuwa ndio kiongozi atakayeleta matumaini mapya.