Friday, 7 February 2014

Uchaguzi kata ya nyasura wilaya ya bunda hatarini kutokufanyika?

UCHAGUZI KATA YA NYASURA WILAYA YA BUNDA HATARINI KUTOKUFANYIKA.


Uchaguzi wa kata ya Nyasura wilaya ya Bunda hatarini kutokufanyika.

Kwa nini?!

1. Nia ni kutaka kumuokoa Mh Wassira na ccm kwa aibu watakayovuna. Kumbukeni wassira alisema chadema inakufa kabla ya 2013, hivyo kushinda kwa chadema kwenye kata hiyo ni sawa na kudhihirisha kuwa Wassira alitumika/anatumika kama tarumbeta la Propaganda.

CCM washambulia mwandishi wa habari vibaya, amri ya Nape? IGP Mangu here is the test

Nimelazimika kukatisha safari baada ya kusikia taarifa za CCM kuanza kutekeleza agizo alilolitoa Nape Nnauye leo mjini Mwanza kwamba Green Guard waanze kufanya kazi yao. Kweli wameanza. Muda mfupi uliopita, Mwandishi wa Habari Christopher Maregesi amepewa kipigo kikali na CCM, huko Bunda. Ilikuwa ni baada ya kitu kinachodaiwa au kuonekana kuwa nimtego kumnasa, kisha watu wa Green Guard, wanaopewa mafunzo kwenye makambi ya CCM yanayoanzishwa kila wakati wa uchaguzi, wakafanya kazi yao.

Baregu aonya kuhusu Bunge Maalumu

8E9U6011
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu amesema, Bunge maalumu lijao la Katiba linaweza kugeuka kituko iwapo wajumbe wake wataweka mbele masilahi ya vyama vya kisiasa na kuacha misingi ya kujenga taifa moja na lenye mshikamano. Pia amesema, pamoja na Tume hiyo ya Mabadiliko ya Katiba kukamilisha kazi yake lakini kwa upande mwingine hatakubali kukaa kimya pindi atakapoona kazi nzuri iliyofanywa ya ukusanyaji maoni ya wananchi ikidhihakiwa.

Mbowe hana shahada ya Chuo Kikuu?

Katika mkutano wa chadema wa M4C pamoja daima uliofanyika tarehe 27 january 2014 ktk viwanja vya barafu jamhuri Dodoma mjini, Tundu Lissu alisema Yafuatayo ..."Ni kweli kuwa mwenyekiti wetu Mbowe hana shahada ya chuo kikuu lakini hiyo sio sababu ya kumnyima uongoz". alisema Lissu juu ya elimu ya Mbowe.

Mbunge Msigwa afikishwa kortini akidaiwa kujeruhi

MBUNGE wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumjeruhi kada wa Chama Cha Mapunduzi (CCM) kwa kitu kitu kizito. Mchungaji Msigwa  alifikishwa  katika mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa, Godfrey Isaya jana na kusomewa shitaka moja la kujeruhi. Akisoma shitaka hilo Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Elizabeth Swai alidai Mchungaji Msigwa alitenda kosa hilo Febrauri 5, 2014 katika kijiji cha Nduli  mjini Iringa. 

Kikwete awaonya wanasiasa

Rais Jakaya Kikwete ametangaza kuwa Bunge Maalumu la Katiba litaanza Februari 18 mwaka huu huku akiwataka viongozi wa vyama vya siasa nchini kuweka mbele masilahi ya Taifa na siyo ya vyama vyao. Rais Kikwete alisema wajumbe 640 wa Bunge hilo wengi ni wafuasi wa vyama vya siasa, hivyo wanatakiwa kukubaliana kwa hoja badala ya kila upande kuvutia kwake.Aliwaonya pia wanasiasa kutokazania suala la muundo wa Muungano peke yake, bali waangalie na masuala mengine yaliyomo kwenye rasimu hiyo ambayo ni muhimu kwa Taifa.

Lema ajisalimisha polisi


MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) amejisalimisha mikononi mwa  polisi mkoani hapa baada ya kutakiwa kwenda kuandika maelezo ya uharibifu wa mali. Lema aliwasili kituoni hapo jana mchana akiongozana na Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Arusha Efatha Nanyaro na viongozi wengine na kuelekea kwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha, OCD Gileas Mroto.

Wednesday, 5 February 2014

Urais CCM kama vita

“Mungu amempa uwezo akisimama watu humfuata nyuma katika kusaidia wanyonge, yeye ana nguvu za Mungu, nadhani hiyo ndiyo inamletea taabu. Sasa mimi niulize kuna kamati za maadili sawa, tangu mwaka 1993 ameanza harambee leo wanasema ameanza kampeni?” alihoji Nangole. Alisema Lowassa amekuwa akisaidia kila pembe ya nchi katika nyumba za ibada na hafanyi kampeni, kwani hao wanaosaidiwa siyo wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM.

Lema Vs Polisi tena Arusha

Polisi mkoani hapa, imetoa notisi ya kukamatwa kwa Mbunge wa Arusha, Godbless Lema (pichani) na wenzake watatu ili kuhojiwa kuhusu malalamiko ya vurugu zilizotokea kwenye mikutano ya kampeni za uchaguzi wa kiti cha udiwani Kata ya Sombetini, wiki iliyopita na kusababisha watu kadhaa walijeruhiwa. Hata hivyo, Mbunge Lema alisema jana kuwa hana taarifa ya kutafutwa polisi kwa ajili ya mahojiano. Alisema kama ni kweli anatafutwa basi taratibu zifuatwe ili aweze kwenda kuripoti polisi.

Tuesday, 4 February 2014

KUMBE LOWASSA NI TISHIO CCM

PATASHIKA nguo kuchanika ni kauli ya kibabe inayoweza kutumika kuelezea sakata la siasa za makundi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM)  linaloshika kasi huku baadhi ya wanachama wakitupiana lawama kwa kuunga mkono upande fulani kuelekea mbio za urais hapo mwakani. Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Ngoyai Lowassa hajawahi kutoa tamko lolote juu ya kugombea urais mwakani lakini shutuma kwamba anautaka zimekuwa zikiibuka kila kukicha.

Njombe: Kada wa CHADEMA avunjwa taya, watatu wawekwa ndani

INASIKITISHA LAKINI IMETOKEA

Katika hali isiyotarajiwa kamanda mmoja wa chadema mkoani njombe amevunjwa taya leo hii katika eneo la matalawe kwenye jimbo la Mama ANNA MAKINDA.

Haya yametokea baada ya kamanda huyo ambaye ni kiongozi wa ulinzi kanda ya nyanda za juu kusini bwana KALONGA kuwafumania viongozi wa chama cha MAPINDUZI wakigawa fedha kwa wananchi ili wawapatie vitambulisho vyao vya kupigia kura.

Kalonga na viongozi wengine walizingirwa na viongozi wa chama mapinduzi na kuanza kupokea kipigo kitakatifu ambacho kilipelekea taya zake kuvunjika vibaya.

polisi walipofika waliwakamata na kuwapeleka kituoni ambapo viongozi watatu wamewekwa ndani huku aliyeumizwa akakicheleweshwa kwa makusudi kupelekwa hospitali huku wakitoa kauli zilizokosa ubinadamu.

Anayeratibu zoezi hili kwa karibu kabisa ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa na mbunge wa jimbo la njombe kaskazini bwana ja people ambaye mudda wote yupo karibu a polisi ili kuhakikisha wanaihujumu chadema

Nitaendelea kuwapa taarifa kwa kadiri ninavyoweza ila kwa sasa narudi polisi kupigania kamanda wetu atoke ili akatibiwe

MUNGU ISIMAMIE CHADEMA

MUNGU ITAZAME TENA TANZANIA


Mpinzani Mpya wa Mwigulu apatikana

Ni Mwanasheria machachari George Kidindima ametangaza nia ya kugombea Ubunge ktk Jimbo la iramba magharibi 2015 kupitia CHADEMA -Kidindima amepata kuwa Mhadhiri msaidizi ktk Chuo ya uhasibu Singida campus pia ni mwandishi wa vitabu kadhaa vya business law.

Stay tune...............

Msekwa: Wapinzani wakiungana wanaweza kuing’oa CCM

Kiongozi Mstaafu wa CCM, Pius Msekwa amesema endapo vyama vya upinzani vikiungana na kuweka mikakati makini ya muda mrefu, vinaweza kuking’oa CCM madarakani. Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na mwandishi wetu jana, Msekwa alisema kwa mtindo wa sasa wa vyama vya upinzani kila kimoja kusimama peke itakuwa ndoto kukishinda CCM. “Kama vyama vya upinzani vinataka kuwe na upinzani wenye nguvu dhidi ya CCM ni lazima viungane vyote. Tena viweke mikakakati ya muda mrefu ya kujiimarisha,” alisema Msekwa kwenye mahojiano hayo. 

CHADEMA wataendelea kutugawa na kutubagua hadi lini?

CHADEMA na ubaguzi ulipitiliza kikomo,walianza na ubaguzi wa ukabila na ukanda ambao kilasiku wanasema ni propaganda za ccm,wakatufundisha watanzania tuvibague vyombo vya habari TBC,UHURU,RAIA MWEMA,MWANANCHI,MTANZANIA,JAMBO LEO NA STARTV.

Wakaendelea tena tumbague ZITTO KABWE tusishiriki na Zitto wala mikutano yake,huko nyuma walitufundisha tuibague nchi yetu na Rais wetu wakati tunaishi Tanzania sijui walitaka tuhamie Rwanda sijui? walitufundisha tuwabague wapinzan bungeni CUF,TLP,UDP NA NCCR.

Leo hii wanatuhamasisha tuwabague wasanii waliojiunga CCM Kweli ni sawa?kesho mtatuambia tusiende Zanzibar sababu kiembesamaki mmepata kura 34,je hamuoni Sudan kusini leo wanabaguana wao kwa wao tena? Acheni dhambi ya ubaguzi sisi ni watanzania tushindane kwa hoja,

Uhamiaji watuhumiwa kuhujumu mgombea Chadema

Mgombea udiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika uchaguzi mdogo kata yaKiboriloni, Manispaa ya Moshi, Frank Kagoma, ameitwa na Idara ya Uhamiaji mjini hapa kwenda kuthibitisha uhalali wa uraia wake ambao unatiliwa shaka. Hata hivyo, Kagoma ambaye anawania kiti hicho akichuana vikali na mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Willy Tulli na mgombea wa UDP, Adon Mzava, amesema hayuko tayari kuitikia wito huo kutokana na kushauriwa na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, kutokwenda hadi hapo chama kitakapotoa maelekezo.

Mbowe amjibu Kikwete

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), FreemanMbowe amemjibu Rais Jakaya Kikwete kwamba asiingize utani katika masuala mazito ya taifa. Mbowe alisema Katiba ya Tanzania, itaamuriwa na wananchi wenyewe na si Chama Cha Mapinduzi (CM) ambacho kimekuwa na mkakati mkali wa kutaka kuua maoni ya wananchi. Mbowe ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja tu baada ya Rais Kikwete kudai amesikia kiongozi huyo wa upinzani akitangaza kutumia nguvu kupata Katiba mpya.

Rais Kikwete: Wanasiasa acheni kuingilia masuala ya kitaalam

Rais Jakaya Kikwete amewataka wanasiasa kuacha kutoa majibu ya kisiasa katika masuala na changamoto za kitaalam na kiufundi. Amesema matatizo na changamoto za kitaalam na kiufundi ziachiwe kutafutiwa majawabu ya kiufundi badala ya kupatiwa majawabu ya kisiasa. Rais Kikwete alitoa rai hiyo mwishoni mwa wiki, wakati akizungumza na wajumbe wa Halmashauri ya CCM ya Mkoa wa Mbeya.