Friday, 7 February 2014

Uchaguzi kata ya nyasura wilaya ya bunda hatarini kutokufanyika?

UCHAGUZI KATA YA NYASURA WILAYA YA BUNDA HATARINI KUTOKUFANYIKA.


Uchaguzi wa kata ya Nyasura wilaya ya Bunda hatarini kutokufanyika.

Kwa nini?!

1. Nia ni kutaka kumuokoa Mh Wassira na ccm kwa aibu watakayovuna. Kumbukeni wassira alisema chadema inakufa kabla ya 2013, hivyo kushinda kwa chadema kwenye kata hiyo ni sawa na kudhihirisha kuwa Wassira alitumika/anatumika kama tarumbeta la Propaganda.

CCM washambulia mwandishi wa habari vibaya, amri ya Nape? IGP Mangu here is the test

Nimelazimika kukatisha safari baada ya kusikia taarifa za CCM kuanza kutekeleza agizo alilolitoa Nape Nnauye leo mjini Mwanza kwamba Green Guard waanze kufanya kazi yao. Kweli wameanza. Muda mfupi uliopita, Mwandishi wa Habari Christopher Maregesi amepewa kipigo kikali na CCM, huko Bunda. Ilikuwa ni baada ya kitu kinachodaiwa au kuonekana kuwa nimtego kumnasa, kisha watu wa Green Guard, wanaopewa mafunzo kwenye makambi ya CCM yanayoanzishwa kila wakati wa uchaguzi, wakafanya kazi yao.

Baregu aonya kuhusu Bunge Maalumu

8E9U6011
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu amesema, Bunge maalumu lijao la Katiba linaweza kugeuka kituko iwapo wajumbe wake wataweka mbele masilahi ya vyama vya kisiasa na kuacha misingi ya kujenga taifa moja na lenye mshikamano. Pia amesema, pamoja na Tume hiyo ya Mabadiliko ya Katiba kukamilisha kazi yake lakini kwa upande mwingine hatakubali kukaa kimya pindi atakapoona kazi nzuri iliyofanywa ya ukusanyaji maoni ya wananchi ikidhihakiwa.

Mbowe hana shahada ya Chuo Kikuu?

Katika mkutano wa chadema wa M4C pamoja daima uliofanyika tarehe 27 january 2014 ktk viwanja vya barafu jamhuri Dodoma mjini, Tundu Lissu alisema Yafuatayo ..."Ni kweli kuwa mwenyekiti wetu Mbowe hana shahada ya chuo kikuu lakini hiyo sio sababu ya kumnyima uongoz". alisema Lissu juu ya elimu ya Mbowe.

Mbunge Msigwa afikishwa kortini akidaiwa kujeruhi

MBUNGE wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumjeruhi kada wa Chama Cha Mapunduzi (CCM) kwa kitu kitu kizito. Mchungaji Msigwa  alifikishwa  katika mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa, Godfrey Isaya jana na kusomewa shitaka moja la kujeruhi. Akisoma shitaka hilo Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Elizabeth Swai alidai Mchungaji Msigwa alitenda kosa hilo Febrauri 5, 2014 katika kijiji cha Nduli  mjini Iringa. 

Kikwete awaonya wanasiasa

Rais Jakaya Kikwete ametangaza kuwa Bunge Maalumu la Katiba litaanza Februari 18 mwaka huu huku akiwataka viongozi wa vyama vya siasa nchini kuweka mbele masilahi ya Taifa na siyo ya vyama vyao. Rais Kikwete alisema wajumbe 640 wa Bunge hilo wengi ni wafuasi wa vyama vya siasa, hivyo wanatakiwa kukubaliana kwa hoja badala ya kila upande kuvutia kwake.Aliwaonya pia wanasiasa kutokazania suala la muundo wa Muungano peke yake, bali waangalie na masuala mengine yaliyomo kwenye rasimu hiyo ambayo ni muhimu kwa Taifa.

Lema ajisalimisha polisi


MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) amejisalimisha mikononi mwa  polisi mkoani hapa baada ya kutakiwa kwenda kuandika maelezo ya uharibifu wa mali. Lema aliwasili kituoni hapo jana mchana akiongozana na Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Arusha Efatha Nanyaro na viongozi wengine na kuelekea kwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha, OCD Gileas Mroto.

Wednesday, 5 February 2014

Urais CCM kama vita

“Mungu amempa uwezo akisimama watu humfuata nyuma katika kusaidia wanyonge, yeye ana nguvu za Mungu, nadhani hiyo ndiyo inamletea taabu. Sasa mimi niulize kuna kamati za maadili sawa, tangu mwaka 1993 ameanza harambee leo wanasema ameanza kampeni?” alihoji Nangole. Alisema Lowassa amekuwa akisaidia kila pembe ya nchi katika nyumba za ibada na hafanyi kampeni, kwani hao wanaosaidiwa siyo wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM.